HII NDIO SABABU SUPERSPORT HAITAONYESHA AFCON

Supersport ambao wanaongoza katika upeperushaji wa habari za michezo ya kimataifa hasa soka wametangaza rasmi leo kuwa hawatakuwa wakipeperusha moja kwa moja mashindano ya Afcon yanayoanza tarehe 13 mwezi huu wa Januari.

Wamiliki Multichoice wametoa taarifa leo kuwa kukosa ruhusa ya kupeperusha matangazo hayo ndio chanzo kikubwa cha kutotangaza soka hilo kubwa la bara afrika.

Supersport yenye makazi yake Afrika kusini inaongoza kwa kuonyesha matangazo ya mashindano makobwa ya Uefa pamoja na  ligi mbalimbali kubwa za ulaya,  hata hivyo wamesema mashindano ya mwaka huu ya Afcon yataonyeshwa katika stesheni ambazo ni washirika wao.