MAREFA WATATU WAKENYA WAMETEULIWA KUSIMAMIA AFCON

Marefa watatu kutoka taifa la Kenya wameteuliwa kusimamia mechi za kombe la AFCON 2023 nchini Morocco ambayo yameairishwa hadi januari mwaka ujao 2024

Peter Kamau Waweru, Gilbert Cheruiyot na mwanadada Mary Njoroge ndio wameteuliwa na shirikisho la kandanda barani Afrika CAF kuwa miongopni mwa marefa ambao watasimamia mechi kadhaa za kombe hilo

Waweru ameteukiwa kutokana na tajriba kubwa ambayo amekuwa nayo kwa mda mrefi.

Ikumbukwe kwamba refa huyo aliendesha AFCON ya maka 2022  kule Cameroon kwenye mechi katiya Comoros na Gabon

Cheruiyot na Njoroge pia wanayo tajiriba kubwa ikifuatiwa kuwa wameendesha mechi mbali mbali barani Afrika zikiwemo mechi za mikoa katika maeneo mbalimbali nchini.