AMBROSE KISOI KUWANIA URAIS FIBA

Ambrose Kisoi ambaye ni katibu mkuu aliyejiuzu kutoka shirikisho la mpira wa vikapu (FIBA) hapa nchini Kenya anasema kwamba sasa analenga kuwania urais wa shirikisho hilo katika chaguzi zijazo.

Akizungumza mjini Malindi katika kaunti ya Kilifi kwenye mechi za ufunguzi  wa uwanja wa mpira wa vikapu uliopo eneo la Cleopatra wikendi hii Ambrose ametupia lawama ukosefu wa ushirikiano baina ya maafisa wenza katika shirikisho hilo jambo lililopelekea yeye kuachana na wadhifa wake.

Kisoi sasa amesema analenga kuwa na majadiliano ya uwazi na kila mshika dau ili kuimarisha mchezo huo tofauti na sasa ambapo anahisi kuna utengano na kama atakuwa rais ataweza kuboresha mambo muhimu kwa mchezo huo wa vikapu.

Wakati hayo yakijiri mkufunzi ambaye pia ni msimamizi mkuu wa mchezo wa mpira wa vikapu katika kaunti ya kilifi maarufu kama BAK mwite Frank Osogo ameweka bayana kuwa lengo lao kubwa kwa sasa ni kuimarisha mchezo huo katika kaunti ya Kilifi.

Amesema kuwa BAK inapania kuupa mchezo huo umaarufu Kilifi kwa mashindano mbalimbali na kushawishi serikali kujenga viwanja vya kutosha vya Basket Ball.