SUBRA YA MIAKA 40 YAFIKA KIKOMO IVORY COAST – KALOE

Solomon Kaloe, mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea anaimani kuwa mashindano ya kombe la Afcon mwakani yatakuwa ya kufana zaidi akiashiria jinsi ambavyo taifa la Ivory Coast limejiandaa kwa ajili ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Mara ya mwisho mashindano ya Afcon yaliandaliwa Ivory Coast ni mwaka 1984, Kaloe ameeleza furaha yake kuwa subra ya miaka zaidi ya 40 imefika kikomo.

”Kuandaa mashindano ya Afcon kwetu ni kitu kizuri. Tumetamani sana kuandaa mashindano haya makubwa ambayo tumeyasubiri kwa miaka 40 na hatimaye subra hiyo imefika kikomo. Tunasubiri sana kuwa wenyeji wa mashindano hayo mwakani ila kukaribisha mataifa yote ya Afrika katika Ardhi ya Soka.”

Mashindano ya Afcon mwakani yataanza rasmi tarehe 13 mwezi January hadi 11 mwezi February, hii ikiwa ni takriban siku 29 kutoka sasa.