GOSHI UNITED YASIMAMISHWA MALINDI

Klabu ya Goshi United inayoshiriki ligi ya eneo bunge la Malindi kaunti ya kilifi imefungiwa na fkf  kushiriki ligi hiyo kwa muda usiojulikana baada ya kupatikana na hatia ya ukosefu wa nidhamu mara kadhaa msimu huu.

Lucas Bahati ambaye ni katibu mkuu wa soka hilo ni kuwa ukosefu mkubwa wa nidhamu kwa klabu hiyo umesababisha fkf kufanya kikao na hatimaye kuja na mwafaka huo kama adhabu.

Awali Goshi walikuwa wamefungiwa kutumia uwanja wao wa nyumbani na kulazimika kucheza mechi zao zote za nyumbani katika uwanja wa Mere.

Lucas Bahati amenukulika katika taarifa rasmi kwa vilabu akisema ,”Baada ya kulikalia kwa makini kama uongozi wa ligi tumeafiki kuwa, kutokana na muendelezo wa ukosefu wa nidhamu kwa Goshi UNited adhabu ya kuifunga ligini itawafaa. Tunatoa wito kwa vilabu vyote mashinani vinavyoshiriki ligi hii kulipa hela za ushirika kwa wakati kipindi cha pili cha ligi msimu huu.”

Wakati uo huo Bahati amewahimiza washiriki wote wa ligi hiyo kukamilisha malipo ya hela za kushiriki ligi hiyo wakati huu ambao raundi ya pili ya ligi imeanza.