TUTASHIRIKI KLABU BINGWA AFRIKA, TUNASTAHILI – RACHIER

Mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia Ambrose Rachier anasema kwamba ako na imani shirikisho la soka barani afrika Caf litabatilisha uamuzi wake wa kuitoa klabu hiyo katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika pamoja na kuitaka fkf kuinyanganya leseni ya ushirika wa fifa klabu hiyo.

Kogalo  wamejipata pabaya kutokana na kuchelewa kulipa wachezaji wake wa zamani hela walizokuwa wanadai licha ya kupewa muda mwingi kukamilisha malipo hayo.

Rachier amethibitisha kwamba amekamilisha malipo yote ya wachezaji hao watatu licha ya kucheleweshwa.

Rachier anaomba shirikisho la soka la CAF kuirudisha Gor Mahia katika orodha ya vilabu vitakavyoshiriki katika mashindano ya klabu bingwa msimu ujao akisema wako na sababu zote za kustahili kucheza mashindano hayo.