GOR MAHIA YAPATA PIGO

Shirikisho la soka barani Afrika CAF  limeamuru shirikisho la soka hapa nchini FKF linaloongozwa na rais Nick Mwendwa kuwapokonya kibali cha ushirika wa fkf klabu ya Gor Mahia ambao ni mabingwa wa ligi kuu yan fkf hapa nchini msimu uliotamatika majuma machache yaliyopita.

Kulingana na taarifa iliyotujia hivi punde ni kwamba klabu ya Gor Mahia imehalifu sheria za CAF za upewaji wa leseni za klabu pamoja na kukosa kulipa wachezaji wao wa awali hela wanazodai licha ya kutoa ahadi za malipo.

Kubwa zaidi Caf imeitoa klabu ya Gor Mahia katika mashindano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao licha ya kwamba walibeba ubingwa wa ligi hapa nchini Kenya na kustahili nafasi hiyo.

Pigo hili pia lingewafuata Kogalo tena katika sheria nyingine ya Caf kwamba walitaka klabu zote zinazoshiriki mashindano ya CAF kuwa na timu ya kinadada huku klabu ya Gor Mahia haina wenzao wa kinadada.