WANYONYI ATOA WITO KWA SERIKALI KUHUSU NDONDI

Daniel Wanyonyi ambaye ni bondia wa Kenya anayesubiri kuvaana na mpinzani wake Karim Mandonga wikendi ijayo ametoa wito kwa serikali kuwa na usawa katika kukuza vipaji.

Amesema kwamba mchezo wa ndondi nchini umebezwa sana na serilali kiasi kwamba mabondia wanajihisi kutengwa.

Ameshauri wadhamini kuingilia kati suala hilo ili kusaidia mchezo huo kupata hamasa hata zaidi na angalau kupata ufuasi kama yalivyo mataifa mengine kama vile taifa jirani la Tanzania.

Wanyonyi na Mandonga watashua ulingoni  lao  katika ukumbi wa sarit expo centre kuandia mwendo wa saa 12 hadi saa tano usiku jumamosi ijayo tarehe 22.