Mkufunzi wa klabu ya Deep Sea kutoka kaunti ya Lamu Athman Pirezi anasema kwamba hawana matumaini ya kupanda daraja ila kwa sasa wanapigania kusalia ligini angalau waendelee kucheza ligi ya daraja la pili msimu ujao.
Akizungumza na Tama La Spoti kupitia njia ya simu Pirezi amesema kwamba msimu wao wa kwanza katika daraja la pili haujakuwa na mafanikio makubwa tofauti na matarajio yao walipopanda kutoka ligi ya mkoa msimu uliopita.
Hata hivyo mkufunzi huyo amesema kwamba kucheza kwao katika ligi kubwa kama hiyo kumegeuza mitazamo ya vilabu vingi mashinani mwa kaunti ya Laumu ikizingatiwa kwamba Deep Sea ndio timu pekee inayoshiriki ligi kubwa.

