Nick Mwendwa ambaye ni rais wa shirikisho la soka hapa nchini amesema kwamba fkf imeanzisha mradi wa kupeana mafunzo kwa marefa wengi pamoja na wakufunzi kama njia maoja ya kukuza mchezo wa soka hapa nchini.
Mwendwa anasema mradi huo utakuwa wa manufaa pia katika mashindano ya Chapa dimba na safaricom yaliyoanza wikendi ilopita katika mkoa wa Magharibi ambapo pia wanalenga kuanza kutafuta wachezaji watakaowakilisha taifa la Kenya katika siku za usoni.
Mashindano hayo ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 yalikuwa yamesimama kwa muda wa miaka mitatu baada ya ujio wa janga la korona 2020 na yalizinduliwa rasmi siku ya jumamosi na shrikisho la soka pamoja na mdhamini mkuu ambaye ni safaricom katika uwanja wa Camp Toyoyo jijini Nairobi.
Nick Mwendwa anasema pia wanalenga kutumia mashindano hayo kuwapa nafasi wachezaji mashinani kuonyesha vipaji vyao. Fainali za mashindano hayo zitakuwa tarehe 14 mwezi januari mwaka 2024.

