Vijana wa mkufunzi Juma Kalato Omax Fc wanazidi kuselelea kileleni mwa ligi ya Fkf katika daraja la pili baada ya jana kusajili ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sparki katika Dimba la ugenini.
Mechi nyingine ilochezwa jana ni ile ya Simba Apparel dhidi ya Kishada fc. Kishada katika uwanja wao wa nyumbani walionyesha ubabe kwa kushinda bao 2-0.
Kufuatia kipigo hicho sasa Simba Apparel imemeweka pengo la alama 8 nyuma ya Omax Fc wanaongoza ligi na alama 57.
Furunzi Fc kufuatia kuandikisha matokeo duni kwa kupoteza mechi tano mfululizo umeshuka hadi nafasi ya mwisho kwenye ligi wakiwa na alama 17.
Hayo yanajiri baada ya klabu hiyo yenye makazi yake Malindi Kaunti ya Kilifi kuachana na mkufunzi wake Nero Chishenga aliyehamia klabu ya Biringi Sharks.

