URUGUAY NDIO MABINGWA WA DUNIA KATIKA MASHINDANO YA U20

Timu ya taifa ya Uruguay ndio mabingwa katika mashindano ya kombe la  dunia ya soka nchini Argentina.

Uruguay wamesajili ubingwa huo baada ya kuilaza italia kwa kichapo cha bao 1-0, bao ambalo limefungwa na Luciano Rodriguez katika dakika ya 86.

Kwengine ni kwamba timu ya taifa ya Israel jana walisajili ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Korea kusini jambo ambalo liliifanya Isreal sasa kumaliza katika nafasi ya tatu ya mashindano hayo.

Mashindano haya yamekuwa na ushindani mkali licha ya kuwa ya vijana wachanga katika soka. Timu ya Afrika kuwa ya mwisho kustahimili makali ya mashindano haya ni Senegal.

Timu za Afrika zilizokuwa katika mashindano haya ni Senegal, Nigeria, Tunisa lakini pia Gambia.