Spika wa bunge la kitaifa nchini Moses Masika Wetanga, ameitaka wizara ya usalama nchini kuwaondelea wanahabari kikwazao, cha wao kutoingia ndani ya msitu wa Shakahola, wakati wakiendeleza zoezi la kufukua miili ya waumini wa kanisa la Good News International, linaloongozwa na mchungaji mwenye itikadi kali Paul Mackenzie.
Kwa mijibu wa spika ni kuwa wakenya kwa sasa, wanahamu ya kufahamu jinsi Mackenzie aliweza kuendeleza mafunzo ya itikadi kali na kusababisha vifo vya halaiki pasi na viongozi wa idara ya salama eneo la Shakahola na kaunti ya Kilifi kwa jumla, kuwa na ufahamu wowote kuhusiana na suala hilo.
Akizungumza katika hafla ya kuwatuza wanahabari nchini ya AJEA, amewapongeza wanahabari kwa kuwa wa kwanza kufichua uovu huo uliokuwa ukiendelezwa katika msitu wa Shakahola, eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Wetangula amesema kuwa ipo haja ya Mackenzie kupewa adhabu kali zaidi huku akiongeza kuwa ipo haja ya wanahabari, kujiotokeza na kuwafichua baadhi ya wale wanaotumia dini, katika kuendekeza itikadi potofu kwenye jamii.
Hata hivyo ameahidi kushirikiana na baraza la wanahabari nchini katika shughuli za kuongozwa wabunge kutunga sheria zitakazo linda uhuru wa wanahabari nchini.
Kulingana na Wetangula ni kuwa baraza hilo liko na uhuru wa kuwasilisha mapendekezo yake kuhusiana na baadhi ya sheria ambazo wanahisi zinapaswa kuidhinishwa ulikufakikisha utuendakazi wa wanahabari katika taifa hili.
Wakati uohuo amewapongeza wanahabari kwa kuendelea kuwa katika mstari wa mbele kuhabarisha na kufahamisha wakenya kuhusiana na matukio mbali mbali huku akisema kuwa wanahabari wanajukumu kubwa zaidi katika taifa hili na wanapaswa kuheshimiwa kwa juhudi zao.
.

