MUUNGANO WA AZIMIO WASITISHA SHUGHULI ZA MAANDAMANO.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umeafikiana kusitisha shughuli za maandamano dhidi ya uongozi wa Rais William Ruto na badala yake kuendeleza mazungumzo na viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza.

Haya yanariji baada ya ombi la muungano wa Azimio la kumtaka mbunge wa Eldas kaunti ya Wajir, Adan Keynan, kuondolewa kwenye kamati Kenya Kwznza katika mazungumzo hayo, kwa kile walichodai kuwa ni kiongozi wa chama cha Jubilee, chana ambacho bado wanadai kiko ndani ya muungano wa Azimio, kwa mujibu wa msajili wa vyama vya kisiasa nchini.

Akizungumza na wanahabari kinara wa walio wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandai, amesema kuwa huenda wakarejelea maandamano hayo iwapo muungano wa Kenya Kwanza, hauta kubaliana na baadhi ya matakwa ya Azimio la Umoja One Kenya, wakati watakapo kuwa wakiendeleza mazungumzo hayo.

Kwa upande wake mbunge Adam Kenynan, amewataka viongozi wa muungano wa Azimo la Umoja One Kenya, kukubali kuendeleza mazungumzo hayo na kuacha kutoa sababu zisizo kuwa na msingi, huku kauli yake ikiungwa mkono na kinara wa walio wengi katika bunge la Seneti Aaron Cheriot, pamoja na Kimani Ichungwa wa bunge la kitaifa na kusema kuwa wako tayari kulegeza masharti yao, ili walete suluhu la malalamishi ambayo yamekuwa yakiibuliwa na muungano wa Azimio la umoja One Kenya.