BARAZA LA MAKANISA NCHINI NCCK LAIONYA SERIKALI DHIDI YA KUWAKANDAMIZA VIONGOZI WA KIDINI.

Mauaji ya halaiki eneo la shakahola yasitumiwe na serekali  kuyalenga makanisa na kupelekea kuundwa kwa sera zitakazo dhibiti maenoeo ya kuabudu humu nchini.

Ni kauli ya mwenyekiti wa Baraza la kitaifa la makanisa humu nchini NCCK tawi la pwani Askofu  Peter Mwero ambaye amesema kuwa ipo haja ya serikali kufanya uchunguzi wa kina na kumkabili Yule aliye tekeleza kinyume cha sheria na ubinadamu.

Mwero amesema kitendo cha uhalifu cha  mhubiri mmoja hakifai kulichafulia jina kanisa nchini kwani sio kila muhubiri katika taifa hili anaeneza imani potofu.

Viongozi hao wameitaka serekali kuharakisha uchunguzi kuhusiana na maujai hayo, yanayomhusisha mhubiri mwenye utata Paul Mackenzi ili haki itendeke.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Kiangilikana dayosisi ya Malindi kaunti ya Kilifi Reuben Shukuru Katite ameyataka makanisa kuwa chini ya miungano ambayo inatambulika kisheria ili kusaidia katika kudhibiti kuenea kwa mafundisho ya imani potovu.