SERIKALI YA BADILI MFUMO WA UFADHILI WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.

Serikali ya kitaifa imebadili mfumo wa ufadhili wa wavyuo vikuu nchini pamoja na taasisi za kiufundi nchini hali ambayo inadaiwa kuleta afueni kwa baadhi ya wanafuni wa taasisi hizo nchini.

Akitangaza mabadiliko hayo baada ya kukoa na wadau wa elimu ya vyuo vikuu na taasisi hizo za kiufundi katika ikulu ya Nairobi, Rais William Ruto amesema kuwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo kuwa na uwezo mzuri wa kifedha, watapata ufadhili wa karo kwa asilimia 53 na mkopo kwa asilimia 40.

Kulingana na rais Ruto ni kuwa wanafunzi wanatoka katika familia ambazo zina uwezo wa kugharamikia karo za wanao ama hata zile zilizo na uwezo mzuri wa kifedha watapata ufadhili wa karo kwa asilimia 38 na mkopo wa asilimia 55.

Kwa wale watakao kuwa wakijiunga na vyuo vya kiufundi wanatarajiwa kupata ufadhili wa serikali kwa asilimia 50 na mikopo ya asilimia 30 huku familia zao zikitakiwa kulipa asilimia 20 iliyosalia.

Aidha Rais amesema kuwa huenda karo ya taasisi hizo ikakosa kuongeza kwa sasa ila hatua ya kuongezeka kwa karo hiyo kutategemea ripoti ya kila mwaka ya shirika la utafiti la KENYA NATIONAL BUREUA OF STATISTICS.