Klabu ya Tottenham Hotspurs imeamua kufidia gharama ya tikiti kwa mashabiki wake baada ya tukio la jumapili ambapo Spers walipigwa kichapo cha aibu cha mabao 6-1 dhidi ya Newcastle United katika uwanja wa St James Park.
Klabu hiyo imetoa taarifa kwamba imehuzunishwa na kipigo hicho ambacho ni chungu kwa mashabiki hivyo kuamua kuwarudishia hela wanunue tiketi za mechi ijayo.
Spurs watakuwa wanashuka dimbani Alhamisi wiki hii dhidi ya Manchester United na uongozi wa klabu hiyo umeahidi mashabiki wake kwamba wanapania kuandikisha matokeo mazuri ili angalau kupunguza machungu ya kipigo cha wikendi ilopita.

