Leeds United katika uwanja wao wa nyumbani Ellan Road walitandikwa kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Crystal Palace huku Arsenal ikikabwa koo na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Kwa matokeo hayo sasa imeshuka hadi nafasi ya nane kwenye ligi huku Arsenal ikiendelea kuselelea kileleni kwa alama 73 alama 6 mbele ya wa pili Manchester City ambao pia wanasalia na mechi moja kiporo.
Kwa sasa Arsenal wanasalia na kibarua kizito kukwachua ubingwa wa ligi kuu ya uingereza msimu kwani bado hawajavaana na Manchester City katika mechi ya marudiano, hii ikizidi kumkosesha usingizi mkufunzi Mikel Arteta kwani kwa sasa amesalia na kombe moja tu la primia.

