YOUNG BULLS YAPOTEZA MECHI YAKE YA KWANZA LIGINI, OMAX IKIZIDISHA UONGOZI WA DARAJA LA PILI

Klabu ya Malindi Young Bulls sasa wamepoteza mechi yao ya kwanza ya daraja la kwanza kitaifa baada ya kutandikwa na Dandora Youth kichapo cha bao 1-0 katika dimba la Komarock jijini Nairobi.

Wakati hayo yakijiri wenzao wa Malindi Progressive academy jana katika uwanja wa Alaskan walisajili ushiondi wa mabao 3-1 dhidi ya wanajeshi wa Kenya navy. 3K FC walipiga sare ya bao 1-1 dhidi ya klabu ya Ruiru Hotsters wakati Buruburu pia walilazimishwa sare ya 1-1 katika uwanja wao wa nyumbani na Vapour Sports.

Gor mahia Youth ilipigwa mabao 2-0 dhidi ya Kibera Soccer na hatimaye wanabenki Equity waliindanika Balaji EPZ kichapo chja bao 1-0.

Katika mechi za daraja la pili kitaifa ni kwamba viongozi wa ligi Omax FC inayoongozwa na mkufunzi Juma Kalato ilisajili ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya Sparki Youth katika uwanja wao wa nyumbani.

Simba Apparel walishinda Samburu Lions kwa kichapo cha 1-0  na hatimaye Kishada katika uwanja wao wa nyumbani wakipigwa na Deep Sea inayoongozwa na mkufunzi Athman Pirezi kichapo cha bao 1-0.