Mechi ya daraja la pili kitaifa kati ya Mariakani Youth dhidi ya Ashton Rangers itakuwa inarindimwa rasmi mchana wa leo (10-4-2023) katika dimba la chuo cha kiufundi cha mariakani mwendo wa saa tisa.
Wakati hayo yakijiri mechi ya vija awa mkufunzi Peter Mole waite Beach Bay iliyofaa kufanyika jana katika uwanja wa mjanaheri sasa imeahirishwa rasmi hadi jumatano wiki hii.
Hii inatokana na changamoto za kiofisi ambazo kulingana na mkufunzi wa Yanga ziliwalazimu kutuma ombi la kuahirisha mechi hiyo ichezwe tarehe 12 mwezi huu wa April.
Kwengine ni kwamba mchezaji wa zamani wa klabu ya Black Stars Fransis Koyugi wa klabu ambayo ni kati ya klabu kongwe mjini Malindi amesajiliwa rasmi na klabu ya Darajani Gogo inayocheza ligi ya National Super League.
Koyugi ambaye ni difenda anatajiriba ya kuchezea klabu ya Wazito Youth kabla ya kusajiliwa na kucheza japo kwa muda mfupi katika klabu ya Mathare United na baadaye kufeli katika jaribio lake la kuchezea klabu ya Malindi Progressive.

