Frank Lampard sasa amepewa kazi ya kukiongoza kikosi cha Chelsea kama mkufunzi wa muda hadi mwisho wa msimu huu.
Hii ni baada ya Chelsea kumfuta kazi mkufunzi wao Graham Potter kutokana na matokeo mabaya msimu huu.
Frank Lampard ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Chelsea alikuwepo Chelsea kama mkufunzi na kufutwa kazi kutokana na kuandikisha matokeo mabaya.
Kwa sasa kibarua chake kikubwa ni mashindano ya klabu bningwa ulaya ambako Chelsea waliingia katika hatua ya robo fainali.

