BARAZA LA CIPK KAUNTI YA TANA RIVER LAMTAKA RAILA ODINGA KUSITISHA MAANDAMANO

Viongozi wa dini ya Kiislamu katika baraza la wahubiri na maimamu CIPK kaunti ya Tana River, wamemtaka kinara wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga kusitisha maandamano ya kila Jumatatu na Alhamisi kuanzia wiki hii kupinga uongozi wa rais William Samoei Ruto.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo tawi la kaunti ya Tana River Sheik Ibrahim Mohammed, maandamano hayo yanaathiri shughuli za maombi ya Aisha, amemtaka Rais William Ruto kuangazia suala la kupunguzwa kwa bei ya bidhaa msimu huu wa Ramadhani kwani idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislamu wameshindwa kumudu bei ya vyakula kutokana na hali ngumu ya maisha.