SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YATENGA FEDHA ZA KUNUA VIFAA VYA MATIBABU

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amesema serikali ya kaunti ya Kilifi imetenga fedha za kununua vifaa vya matibabu, katika hospitali ya Marafa eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo tayari wameagiza zaidi ya vitanda 100 vya kusaidia wagonjwa, watakokuwa wakilazwa katika kutuo hicho cha afya.
Kulingana na gavana huyo hospitali hiyo, inaupungufu wa vifaa muhimu vya kiafya, suala analosema limepewa kipaumbele na serikali yake.
Wakati huohuo amebainisha kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kupeleka madakatari wa upasuaji katika kituo hicho cha afya na pia madaktari wa magonjwa mengine wanaohitajika kwani hospitali hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi wiki sita zijazo ili kuwahudumia wakazi wa eneo bunge hilo la Magarini.