Ipo haja ya wananchi pamoja na viongozi wa kijamii katika eneo la Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla, kushirikiana ili kutatua baadhi ya changamoto za kiusalama katika jamii.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa mipango katika shirika la kijamii la kuangazia usalama na amani la KECOSCE Maxwell Lumbasi, ambaye ametaja ukosefu wa ajira na usalama katika wadi ya Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi, kuendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza baada ya kufanya kikao na wananchi katika eneo hilo la Shella, Lumbasi amesema wapo baadhi ya viongozi wa kijamii ambao tayari wamekuwa wakijiotokeza kusaidia katika kuleta suluhu la kudumu kuhusiana na suala hilo.
Kwa upande wake afisa mkuu katika kitengo cha dhuluma za kijinsia kwenye hospitali ya eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi Prudence Kombe ameeleza kuwepo kwa umuhimu wa dhuluma za kijinsia dhidi ya watu wenye uatilifu kuangaziwa katika eneo hilo.
KECOSCE YAWATAKA WENYEJI WA KAUNTI YA KILIFI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KIJAMII

