Mwenyekiti wa jamii ya Wamakonde kaunti ya Kwale Thomas Nguli amesema jimii hiyo eneo bunge Msambweni imekuwa ikitengwa na serikali ya kaunti hiyo kwenye masuala ya ajira.
Nguli amesema licha kutambuliwa rasmi kama Wakenya hawajakuwa wakihusishwa katika masuala ambayo yanahusu serikali ya kaunti ya Kwale.
Aidha, ameipongeza serikali ya kitaifa kwa kuwatambua na kuwapa nafasi zaidi katika kitengo cha idara ya usalama nchini akisema ni hatua ambayo inaendelea kuimarishia maisha yao kwa kiwango kikubwa.
Nguli ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ameipongeza serikali ya kitaifa kutokana na kile ambacho amesema imeitambua Jamii ya Wamakonde kwa kuwapa vitambulisho vya kitaifa pamoja na hatimiliki za ardhi ambazo wanaishi.
JAMII YA WAMAKONDE KAUNTI YA KWALE YADAI KUTENGWA

