Wakulima kaunti ya Kilifi wametakiwa kupanda mimea ambayo huchukua mda mfupi kukomaa shambani, kutokana na kuwepo kwa mvua chache ambazo zinatarajiwa kushuhudiwa katika kaunti ya KIlifi.
Haya ni kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya Kilifi, ambayo imeeleza kuwa ipo haja ya wakulima kushirikiana na maafisa wa kilimo nyanjani ili kupewa mwelekeo unaofaa kuhusiana na mimea hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa idara hiyo kaunti ya Kilifi Geoffrey Ogutu amewaonya wananchi dhidi ya kupanda mahindi kwa wingi kwani huenda ikakosa kufanya vyema.
Aidha, amesema wakulima pamoja na wananchi wanaopania kutekeleza kilimo msimu huu wanapaswa kuanza shughuli za kutayarisha mashamba yao kwa wakati.
WAKULIMA KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA KUJIANDAA KWA SHUGHULI ZA UPANZI

