Kinara wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa kutakuwa na maandamano kwa jina Unga revolution kila siku ya jumatatu baada ya maandamano ya jana jijini Nairobi na maeneo mengine ya taifa hili.
Raila amesema kuwa maandamano hayo yanalenga kushinikiza serikali kushughulikia kupanda kwa gharama ya maisha akisema kuwa kila siku ya jumatatu itakuwa ni siku ya mapumziko ili kupisha maandamano hayo
RAILA ODINGA ASEMA MAANDAMANO YATAENDELEA KILA SIKU YA JUMATATU

