Mbuge wa Malindi kauntI ya Kilifi Amina Mnyazi amesema anapinga mapenzi ya watu wa jinsia moja nchini.
Akizungumza bungeni alipokuwa akichangia muswada ambao ulikuwa umewasilishwa bungeni kupinga uhalalishaji wa Ushoga na Usagaji nchini, Mnyazi amesema mila na tamaduni za kiafrika, dini na katiba ya nchi haziruhusu Mapenzi ya jinsia Moja na ni suala ambalo linapaswa kupingwa vilivyo.
Mnyazi amesema taifa la Kenya litasimama kidete katika kupinga ushoga na Usagaji nchini akisema suala hilo linaendelea kuwapotosha vijana wengi kimaadili na Wakenya wanapaswa kupinga uovu huo.
Aidha, Mnyazi amesema kutokana na ugumu wa maisha nchini huenda usagaji na ushoga ukatumika katika kuwashawiji vijana ili kujiingiza katika uovu huo na kusisitiza haja ya Wakenya kushirikiana katika kupinga suala hilo kufanikishwa nchini.
AMINA MNYAZI AWATAKA WAKENYA KUENDELEA KUPINGA UHALALISHAJI WA MAPENZI YA WATU WA JINSIA MOJA

