Mwenyekiti wa mashirika ya kijamii kanda ya Pwani Zedekiah Adika amesema mizozo mingi ya umiliki wa ardhi ya umma hutokea kutokana na waliokuwa wamesajiliwa mwanzoni kama wenyeji kufariki au hata kuzeeka.
Akizungumza na LULU FM, Adika amesema baadhi ya watu hutaka kumiliki ardhi hizo na hata kuchukua hatua ya kuziuza pasipo kuwahusisha wakazi wengine katika ardhi hizo.
Aidha, Adika amesema baadhi yao hupeana mashamba hayo kwa familia zao kama urithi na mwishowe kusababisha mizozo hiyo.
Adika amesema ardhi hizo huwa katika hatari ya kunyakuliwa na mabwenyenye kutokana na mizozo hiyo huku akisema mashirika ya kijamii inaendelea kuweka mikakati kuhakikisha ardhi hizo zinalindwa dhidi ya unyakuzi.
MIZOZO MINGI YA UMILIKI WA ARDHI YA UMMA HUTOKANA NA WALIOKUWA WAMESAJILIWA KUAGA DUNIA AU HATA KUZEEKA

