SAMUEL GONZI RAI AWATAKA VIONGOZI WA KWALE KUSHIRIKIANA

Mbunge wa Kinango kaunti ya Kwale Samuel Gonzi Rai amewataka viongozi wa kaunti hiyo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana ili kuiboresha kaunti hiyo.
Rai akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika shule ya msingi ya Kinango amesema ni kupitia ushirikiano ndipo miradi itatekelezwa kwenye kaunti ya Kwale.
Aidha, amesema atahakikisha miradi ambayo ilianzishwa na mtangulizi wake Benjamin Dalu Tayari anaikamilisha.
Naye Fatuma Masito ambaye ni mwakilishi wa kike katika kaunti hiyo amesema wametenga fedha za miradi ambayo inapania kuwainua Vijana na wanawake na kuyataka makundi ya vijana na wanawake kufika kwenye ofisi za NGAAF ili kuchukua mikopo ya kuwawezesha kujiendeleza kimaisha.