Kadi nyekundu aliyopewa Casemiro katika mechi ya jana Manchester United walipokuwa wanavaana na Crystal Palace dimbani Old Trafford sasa itamlazimu kukosa mechi nne mfululizo kutokana na kupewa kadi nyekundu hivi majuzi.
Casemiro alipigwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi kiungo Carlos Alcaraz katika dakika ya 34 baada ya tathmini ya kutosha kutoka kwa refa wa VAR.
Casemiro sasa atakosa mechi ya FA dhidi ya Fulham wikendi ijayo, mechi ya Brentford, Everton alikini pia mechi ya Newcastle United ugenini.
Kadi hiyo haiathiri mashindano ya klabu bingwa Uropa na kiungo huyo atapatikana katika mechi yao dhidi ya Real Betis.

