WEZESHENI KINADADA, JUMBA ASHAURI VIONGOZI

Wito unazidi kutolewa na viongozi wa michezo katika mkoa wa pwani kwa serikali za ugatuzi lakini pia zile za kitaifa kumuangazia mwanadada michezoni ili kuleta usawa katika makuzi ya talanta.

Alizungumza na Tama la Spoti Jumba Alex ambaye ni katibu mkuu wa vilabu vya Malindi Progressive Academy anasema kwamba ipo haja ya kuwaunga mkono vijana wa kike michezoni na kufanya vilabu vya wanadada kuongezeka tofauti na hali iliyoko kwa sasa ambapo kuna uhaba wa vilabu vya wasichana hasa kwenye soka.

Katibu huyo ameshauri viongozi wa vilabu mbalimbali vya mashinani kuanzisha vilabu vya kinadada kama njia moja ya kutoa hamasa na kuwapa motisha wanadada kuingia viwanjani kukuza vipaji vyao ambavyo huenda vikawapa ajira.
Amesema kwamba ipo haja ya viongozi wa vilabu kufuata sheria za michezo ambazo zinafungamana na kuwepo kwa vilabu vya wasichana katika kila klabu ya wanaume ili kuleta usawa.