Washtakiwa watatu wa upangaji wa matokeo wameachiliwa kwa bondi ya shilingi laki tatu kila mmoja baada ya kuwasilishwa mahakamani hii leo.
Akhiad Kubiev raia wa Urusi, Bernard Nabende na Kenyan Martin Munga wote ambao ni raia wa Uganda wameachiliwa baada ya kukamatwa usiku wa ijumaa walipokuwa wanapanga dili ya kupanga matokeo ya mechi ya sofapaka dhidi ya klabu ya Nairobi City Stars.
Watatu hao walikuwa na lengo la kuwahonga wachezaji wa City Stars milioni 1.8 kama malipo ya kufanikisha dili hilo lakini walikamatwa usiku wa manane na maafisa wa polisi ambao walikuwa wamedokezewa kisiri mpango huo na maafisa wa klabu ya City Stars.
Uongozi wa City Stars kupitia Patrick Korir ambaye ni mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo umetoa wito kwa bunge la kitaifa kubuni sheria mathubuti za michezo zitakazotumika kuadhibu wahalifu ambao wanaharibu soka la taifa hili.

