SHEIKH TWAHA OMAR AMKOSOA RAIS WILLIAM SAMOEI RUTO

Mwenyekiti wa chama cha Wiper kaunti ya Mombasa Sheikh Twaha Omar amemkosoa Rais William Samoei Ruto akidai teuzi zake katika nafasi mbalimbali serikalini ni za kibaguzi.
Twaha amepinga uteuzi wa nahodha William Kipkemboi Ruto kama mkurugenzi wa bandari ya Mombasa.
Ameutaja uteuzi huo kama wa kikabila na ubaguzi na kusema kulipaswa kuteuliwa mtu ambaye anatoka kanda ya pwani.
Kauli yake imeungwa mkono na naibu mwenyekiti wa chama cha KANU kaunti ya Mombasa Luka Ombati ambaye amesema ukabila ambao unaendelezwa nchini na Rais William Samoei Ruto huenda ukaathiri shughuli nyingi nchini.
Naye Rahma Godana ambaye ni mratibu wa chama cha UPIA kanda ya pwani ameeleza kutamaushwa na namna baadhi ya watu wanavyobanduliwa katika nyadhifa mbalimbali kwenye tume na mashirika ya umma na nafasi hizo kukabidhiwa wandani wa Rais Ruto.