MONICAH MARUBU ATAKIWA KUOMBA MSAMAHA

Mwenyekiti wa shirika la Lamu Women Alliance Raya Famau amewahimiza viongozi wa kisiasa kutotumia maneno ambayo yatasababisha migawanyik katika jamii kaunti ya Lamu.
Raya Famau amemkosoa mwakilishi wa kike kaunti ya Lamu Monica Marubu kufuatia semi zake majuma mawili yaliyopita wakati wa ziara ya Rais William Ruto kwenye kaunti ya Lamu kuwa ukosefu wa usalama katika kaunti hiyo unasababishwa na maswala ya ardhi.
Amesema ni vyema kwa viongozi kuwaunganisha wananchi na sio kutoa semi ambazo zinaweza kusababisha chuki miongoni mwa wenyeji.
Kauli yake imeungwa mkono na kiongozi wa kina mama kisiwani Lamu Amina Kale ambaye ametoa wito kwa Monicah Marubu kutumia lugha ya kuwaunganisha wakaazi wa Lamu na sio kuwatenganisha na kumtaka kuomba msamaha kufuatia matamshi hayo yako.