Wazazi katika kaunti ndogo ya Kisauni kaunti ya Mombasa wamehimizwa kudumisha ushirikiano baina yao kama mbinu mojawapo ya kuwalea wanao kwa maadili.
Ni wito uliotolewa na wazee wa mitaa wa kike kwenye kikao kilichoandaliwa na shirika la kijamii la kecosce, ambapo wazazi kwa jumla wametakiwa kushirikiana kwani ukosefu wa ushirikiano umetajwa kusababisha baadhi ya watoto kupotoka kimaadili.
Aidha, wamewalaumu wazazi wa kiume kwa kutelekeza majukumu ya malezi ya watoto wao na kuwaachia wazazi wa kike.
Asha Soud ni mzee wa mtaa kaunti ndogo ya Kisauni.
Aisha Wambui ambaye ni mzee wa mtaa eneo la Utange amesema kuwa wazazi wote wanajukumu la kuwafatilia wanao hasa wanapotumia mitandao kwani wengine wao kujifunza tabia za kuwapotosha kimaadili kupitia mitandao.
HIMIZO LATOLEWA KWA WAZAZI ENEO LA KISAUNI KUDUMISHA USHIRIKIANO BAINA YAO

