ASILIMIA CHINI YA MBILI YA WANAFUNZI HAWAJAJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Kwale Ahmed Mohamed Abdi amesema kuwa ni asilimia chini ya mbili pekee ya wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza kaunti hiyo.
Abdi amesema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi kwa sasa wamejiunga na kidato cha kwanza huku akidokeza kuwa ni wanafunzi wachache pekee ambao pia kesi zao zinashughulikiwa kubaini ni kwanini hawajijiunga na kidato cha kwanza hadi kufikia sasa.
Mkurugenzi huyo amesema wanafunzi ambao hawajaenda shule kufikia sasa ni wale wa maeneo ya mashinani hasa yanayokumbwa na ukame na athari za mabadiliko ya hewa.