GAVANA ANDULSWAMAD SHARIFF NASSIR AMEAHIDI KUWATETEA WENYEJI WALIOFURUSHWA KATIKA NYUMBA ZA KUPANGA ENEO LA BUXTON

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kuwatetea wakaazi waliofurushwa katika nyumba za kupanga eneo la Buxton kaunti ya Mombasa.
Katika kikao na waandishi wa habari afisini mwake Nassir amesema amewaandikia barua washikadau wote Pamoja na afisa katika idara husika kuhakikisha wanatoa maelezo kamili kuhusiana na ombi lililotolewa na wakaazi wa nyumba hizo.
Wenyeji hao walikuwa wamewasilisha ombi lao kwa bunge la kaunti kutaka lalama zao kusikizwa ili wapate haki.
Aidha, Nassir ameahidi kuwa wenyeji hao watapata haki yao huku akilitaka bunge la kaunti ya Mombasa kuharakisha uchunguzi wa ripoti iliyowasilishwa na wakaazi hao.
Ikumbukwe kuwa wakaazi hao walifurushwa ili kupisha mradi wa ujenzi wa nyumba za kupanga na za bei nafuu unaotekelezwa na serikali.