Klabu ya thika Bidco United imelazimishwa sare tasa dhidi ya Nairobi City Stars katika mechi ya ligi kuu ya FKF primia iliyochezwa katika uwanja wa manispaa ya Thika.
Matokeo hayo sasa yanaifanya Bidco United kupanda na alama moja hadi nafasi ya 11 ligini wakiwa na alama 23 baada ya mechi 18 huku Nairobi City Stars ikipanda hadi nafasi ya 16 ligini na alama 13 pekee wakiwa katika sehemu hatari ya kushuka daraja.
Antony Akhulia ambaye ni mkufunzi wa klabu hiyo ya kaunti ya kiambu amesema msimu huu anawekeza sana nguvu za klabu yake kwa sasa kuandikisha matokeo mazuri ya ligi pamoja na mashindano ya kombe la Mozzert Bet ambako analenga kufika fainali baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano ya mwaka 2021.

