Wanaume wengi kaunti ya KIlifi hawajakuwa wakijukumika katika kuzingatia afya ya uzazi kwa wake zao wakati wanapokuwa na ujauzito.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa afya ya jamii katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, Edwin Ogoma ambaye ametaja suala hilo kuwa changamoto kuu kwani wengi wa wanaume hao hukosa kufahamu umuhimu wa wake zao kuhudhuria kliniki wakati huo.
Akizungumza na Lulu fm amesema idadi kubwa ya wanawake hupachikwa mimba wakiwa na umri mdogo, suala ambalo pia huchangia kwa wao kukosa kuwa na uwazi wa kuelezea wale waliohusika katika kuwatunga mimba.
Vilevile, amesema suala hilo limechangia kushuhudiwa kwa mizozo kati ya wanandoa, kwani wanaume wengi hudai kutimiziwa mahitaji ya kingono kwa lazima licha ya akina mama hao, kutakiwa kujitenga na suala la kushiriki kitendo hicho cha ndoa, baada ya wao kujifungua kwa njia ya upasuaji.
IDADI KUBWA YA WANAUME KAUNTI YA KILIFI HAWAJAKUWA WAKIJUKUMIKA KUZINGATIA AFYA YA UZAZI KWA WAKE ZAO

