PETER SHAKE ASEMA HAUNGI MKONO MAANDAMANO YA MUUNGANO WA AZIMIO LA UMOJA ONE KENYA

Mbunge wa Mwatate kaunti ya Taita Taveta Peter Shake amesema hatua ya baadhi ya wanasiasa wa Azimio La Umoja One Kenya kujiunga na ule wa Kenya Kwanza inatokana na msukumo wa maendeleo katika maeneo ambayo wanawakilisha.
Akizungumza katika eneo bunge lake La Mwatate Shake ambaye ni mwanachama wa chama cha Jubilee amesema haungi mkono harakati za Raila Odinga kuandaa maandamano na kusema yataathiri shughuli mbalimbali nchini.
Amesema huu ni muda wa waliochaguliwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufanikisha ahadi ambazo walizitoa wakati kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka jana wa 2022.