Uongozi mbaya katika kaunti ya Kilifi ni kati ya changamoto sugu inayosibu michezo katika eneo hili.
Akizungumza na Lulu Fm Bwana Tom Lango ambaye ni mwenyekiti wa fkf eneo bunge la Malindi amesema uongozi wa serikali ya kaunti ya Kilifi uliopita ulikosa kutumia mamilioni ya pesa za michezo katika miradi tofauti licha ya kuafikiana na wadau wa michezo katika mikutano ya hadhara ya kuchukua maoni.
Tom Lango anahoji kwamba hakuna sheria zinazosaidia utoaji au utengaji wa bajeti ya pesa za michezo, jambo ambalo linakera wanamichezo wengi kwa sasa.

