Mbunge wa Garsen kaunti ya Tana River Ali Wario Guyo, amewashauri wakaazi wa Tana Delta kuthamini kilimo nyunyizi kama mbinu ya kukabiliana na baa la njaa.
Guyo amesema upanzi kupitia kilimo nyunyizi utaimarisha uzalishaji wa chakula ikizingatiwa kwamba hali ya kiangazi imesababisha kuadimika kwa mvua.
Aidha Guyo amewakosoa baadhi ya makundi ambayo yalipewa mitambo ya kupandisha maji mashambani na kuishia kuitumia visivyo.
Wakati huohuo Guyo amesema mradi wa shamba la Tarda huko Gamba umetengewa shilingi milioni 620 akisema wenyeji watapata mashamba wakisaidiawa na serikali ili kutekeleza kilimo.
Ni kauli iliyoungwa mkono na mkurugenzi wa wafanyikazi Tana River Mwajuma Habwoka Hiribae ambaye amesema kilimo nyunyizi kitasaidia kukabiliana na baa la njaa.
Hiribae amesema wafugaji wanapaswa kupanda nyasi kwa minajili ya mifugo wao kutumia maji ya mito.
ALI WARIO GUYO AWASHAURI WENYEJI WA TANA DELTA KUTHAMINI KILIMO NYUNYIZI

