ANSELM MWADIME AWATAKA WAZAZI KATIKA KAUNTI YA TAITA TAVETA KUWAJIBIKIA MAJUKUMU YAO YA ULEZI KWA WATOTO WAO

Wazazi kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kuhakikisha wanawajibikia majukumu yao ya ulezi kama vile kuhakikisha watoto wao wanapata haki ya elimu.
Ni wito uliotolewa hasa kwa wazazi ambao watoto wao wanafadhiliwa na serikali ya kaunti kuhakikisha ada ndogondogo zinazotolewa shuleni haziwi sababu ya watoto wao kukosa masomo.
Kwa mujibu wa naibu spika wa bunge la kaunti hiyo ya Taita Taveta, Anselm Mwadime ,wazazi wanapaswa kuwajibikia mahitaji madogomadogo ya waatoto wao ili wawe shuleni baada ya serikali kuwaondolea mzigo mkubwa wa karo.
Aidha, Mwadime amesisitiza haja ya wazazi hao kuwahimiza watoto wao kutia bidii masomoni kwani pindi watakapofeli huenda wakakosa ufadhili huo kutoka kwa kaunti ya Taita Taveta.