VISA VYA MATATIZO YA KIAFYA VINAENDELEA KUATHIRI BAADHI YA VIJANA KANDA YA PWANI

Idadi kubwa ya visa vya matatizo ya kiafya kwa baadhi ya wenyeji wa Pwani, vimechangiwa zaidi na suala la wao kushauriwa kutotumia madawa wamapougua.
Haya ni kwa mujibu wa afisa katika shirika linalohusika na masuala ya kudhibiti magonjwa mbalimbali nchini la NATIONAL SYNDEMIC DISEASES CONTROL COUNCIL, Ezekiel Mwabili  ambaye amesema wagonjwa wengi wamekuwa wakipotoshwa na usharui huo kutoka kwa viongozi wa dini mbalimbali katika jamii.
Akizungumza na mwanahabari wetu Mwabili amesema wagonjwa wengi wamekuwa na dhana kuwa huenda wakapona kupitia maombi na tiba za kiasili badala ya kupata matibabu na mwishowe kuathirika kiafya.
Aidha, ametoa wito kwa jamii kuhakikisha inatathmini taarifa zozote kuhusiana na tiba ya maradhi yanayowakabili ili kupata mwelekeo unaostahili na ambao utawasaidia kupata afueni ya magonjwa wanayougua.