Wito umetolewa kwa viongozi wa michezo nchini kuingia mashinani kutazama na kutambua talanta za wachezaji kama njia moja ya kutimiza lengo kuu la ugatuzi kwa kuangazia wachezaji walio mashinani zaidi.
Jambo hilo litasaidia kutoa hamasa zaidi kuhusu mradi wa serikali wa talanta hela pamoja ambapo vijana wengi wenye vipaji watatambulika.
Akizungumza na Tama La Spoti mkufunzi wa Kilifi Starlets Joyce Unda amelalamika kwamba viongozi wa soka wamekosa kuingia mashinani vilivyo kutoa hamasa na baadhi ya wakufunzi wanakosa matumaini ya kufaidi kutokana na mradi wowowte wa serikali hama huo wa Bottom Up tournaments pamoja na Talanta hela.

