Mkurugenzi wa mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi nchini IPOA kabda ya pwani Hussein Aden amethibitisha kupokea jumla ya kesi 467 kote nchini za malalamishi kutoka kwa wakenya yanayohusiana na maafisa wa polisi tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023.
Kulingana na Hussein kati ya kesi hizo, kesi 67 zimenakiliwa kanda ya pwani na kuwataka maafisa wa polisi kutekeleza majukumu yao kwa wanachi kwa kumujibu wa sheria ya nchi.
Hussein amewaonya maafisa hao na kusema Mamlaka ya IPOA haitamsaza afisa yeyote wa polisi ambaye atapatikana kutekeleza visa vya dhuluma za kibinadamu.
Amehimiza ushirikiano mwema kati ya Wakenya na asasi za usalama ili kuimarisha usalama katika taifa hili la Kenya.
Vilevile, ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanazingatia sheria ya nchi kama inavyopaswa na kuwahimiza kuripoti visa vyovyote vya dhuluma za kijinsia ambavyo vinatekelezwa na maafisa wa polisi dhidi ya wananchi ili wahusika wakabiliwe kisheria.
KESI 67 ZA MAAFISA WA POLISI KUWADHULUMU WAKENYA ZIMENAKILIWA KANDA YA PWANI

