WAZIRI WA USALAMA NCHINI KITHURE KINDIKI AZURU KAUNTI YA KILIFI

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amesema idadi kubwa ya wanafunzi kanda ya pwani ambao wanapaswa kujiunga na kidato cha kwanza wangali nyumbani.
Akizungumza akiwa Gotani eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi, Kithure amesema wanafunzi hao wanapaswa kujiunga na shule za upili ili kuendeleza masomo yao.
Kufuatia hilo sasa amewaagiza Manaibu wa Makamishna pamoja na wasaidizi wao kuzuru mashinani ili kuwatafuta wanafunzi hao wajiunge na shule za upili.
Hatahivyo akizungumzia Disco Matanga Kindiki ameahidi kuweka juhudi zaidi ili kukabiliana na nayo ili kudhibiti visa vya mimba za utotoni.