GAVANA ANDREW MWADIME ASEMA JITIHADA ZINAWEKWA KUHAKIKISHA KUNA MAJI KAUNTI YA TAITA TAVETA

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta inafanya kila jitihada kuhakikisha kuna maji katika kaunti hiyo ili kuwaepusha wenyeji dhidi ya kuhangaika wakisaka maji.
Haya ni kwa mujibu wa Gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime, ambaye anasema kaunti ya Taita Taveta ina mchanga mzuri kwa ajili ya kilimo, lakini changamoto kubwa kwa sasa ni ukosefu wa maji.
Mwadime amesema watashirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili wananchi wapate maji kwa wingi, hasa eneo bunge la Mwatate na Voi katika kaunti hiyo ya Taita Taveta.