SERIKALI YA CANADA YATOA UFADHILI WA SHILINGI BILIONI MBILI

Serikali ya Canada imetoa ufadhili wa shilingi bilioni 2 ili kufanikisha masomo ya kiufundi katika vyuo vya mafunzo ya anuai nchini Kenya.

Akizungumzia ufadhili huo waziri wa masuala ya Kigeni Daktari Alfred Mutua amesema serikali hiyo ya Canada imeahidi kuongeza shilingi bilioni 2 zaidi ili kuboresha masomo hayo na pia kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa kujiajiri wenyewe.

Akizungumza baada ya kuzuru chuo cha Ufundi cha Anuai cha Kenya Coast eneo la Tononoka kaunti ya Mombasa, Mutua amesema serikali kuu itaboresha ushirikiano wa kimataifa ili kuwawezesha vijana kujiendeleza kimasomo.

Kulingana na Alfred Mutua Vijana ambao watafuzu kwenye masomo hayo ya kiufundi watawezeshwa kujiajiri wenyewe, kuajiriwa nchini Kenya na pia kunufaika na nafasi za ajira kwenye mataifa ya nje.